Jumatatu, 31 Desemba 2018

WAARABU WA KUIZIMA SIMBA SC KLABU BINGWA AFRIKA.

Mabingwa wa Ligi kuu Bara nchini Tanzania timu ya Simba Sports Club ya jijini Dar es Saalam wiki iliyopita imefanikiwa kutinga hatua ya Makundi ktk michuano ya Kimataifa ya kuwania ubingwa wa Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Simba SC imefikia hatua hiyo baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Nkana FC ya nchini Zambia majuma mawili yaliyopita katika mchezo wa marudiano uliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Daalam...,kwa kuichapa Nkana jumla ya bao 4 kwa 3,ikiwa ni bao 2-1 Waliyoshinda Nkana kule Zambia na 3-1 waliyoshinda Simba jijini Dar es Salaam.

Matokeo haya yakaipa Simba kibali cha kutinga hatua ya makundi ambapo Ijumaa ya juzi baada ya droo ya makundi kuchezeshwa timu hiyo ya Simba ikajikuta imo kundi D ikiwa ni moja kati ya timu 4 zinazounda kundi hilo.
Katika kundi hilo kuna timu 2 za Uarabuni ambazo ni Al Ahly ya Misri na JS Soura ya Algeria huku timu zingine 2 katika kukamilisha timu 4 katika kundi D zikiwa ni AS Vita pamoja na Simba yenyewe.

Kwa mara kadhaa wababe wa Soka nchini Tanzania klabu za Simba,Yanga na Azamu wamekuwa wakishindwa kutamba mbele ya timu zitokazo falme za Kiaarabu na hasa katika michezo mbalimbali pindi timu hizo zikicheza katika viwanja vya nchi mwao(Uarabuni)

Viongozi,Wanachama,Wachezaji na Mashabiki wa timu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Saalam wanasisituza kwamba mwaka wao huu hivyo wanawaonesha Waarabu kabumbu la aina yake na hasa ukizingatia wana kikosi kipana na chenye uwezo wa kushinda mahali popote.

  Timu ya Simba inaundwa na wacheza wengu,nguli na wenye majina makubwa Afrika Mashariki na kati kamq vile M.Kagere,E.Okwi,C.Chama,S.Kichuya,P.Wawa,A.Manula,S.Kapombe,Mo,Dilunga,Kotei,Boko na wengine wengi.

Hata hivyo timu ya Simba bado ina kibarua kingine cha kuhakikisha walau inatinga robo fainali katika michuano hiyo ili kujihakikishia kucheza tena hapo mwakani kwani hivi juzi imeondolewa katika ligi ya kombe la shirikisho na timu ya daraja la kwanza iitwayo Mashujaa toka pale mkoani Kigoma.
Tunasema hayo kwa sababu hata katika ligi kuu Bara hapa nyumbani mahasimu wao wakubwa timu ya Yanga wanaonekana kuupania vema ubingwa wa mwaka huu kwani hadi sasa wameshajikusanyia pointi 50 kibindoni katika jumla ya michezo 18 waliyocheza  bila kupoteza hata mmoja huku wakishinda michezo 16 na kutoka sare 2 na kufanya waongoze ligi huku wakiwa wamebakiwa na mvhezo 1 ili wafunge mzunguko wa kwanza mbele ya Azam wenye point 40 kwa michezo 17 waliyocheza huku Simba wakiwa nyuma na pointi zao 33 walizokusanya katika michezo14 waliyocheza na wakiwa na kiporo cha mechi 6 mkono kukamilisha mzunguko wao wa kwanza katika ligi kuu Bara.

Mungu ibariki Simba Sports Club
Mungu ibariki Tanzania.
Kila lakh

Hakuna maoni: