Jumapili, 21 Oktoba 2018

CHEKELEA UONGEZE SIKU ZA KUISHI.

Uswahilini kuna vituko.
Vunja mbavu kidijitali.

SIMBA WAMPA POLE MO DEWJI KWA KUICHARAZA STAND UNITED 3-0

Hii leo kunako dimba la Taifa kumeshuhudiwa mchezo wa nguvu ukiwakutanisha mabingwa watetezi Simba SC ya jijini Dar es Saalam dhidi ya Stand United ya Shinyanga.
Ambapo hadi dakika 90 za mchezo kumalizika Simba ilitoka kifua mbele kwa ushindi mnono wa magoli 3 kwa 0 huku magoli hayo yakitiwa kimiani na wachezaji  Cletous Fhama mnamo dakika ya 30 wakati la pili likifungwa na Emmanuel Anord Okwi huku lile la 3 likiwa ni la kujifunga Stand Utd wenyewe baada ya kutokea harakati za uokoaji wa mpira wa kona ulipigwa na Shiza Ramadhan Kichuya mnamo dakika ya 86 ya mchezo.

Kwa ushindi huo ni kudhihirisha kwamba kile walixhokieleza wachezaji kabla mchezo huu hapo jana ni kwamba watashinda mechi hiyo ya kesho(leo)ili iwe ndiyo pole yao kwa Boss wao aliyekuwa kapotea kwa kutekwa kwa zaidi ya siku 8 kabla ya kupatikana usiku wa kuamkia jana.

Mbali na hivyo Simba watakuwa wameendelea kujiweka pazuri zaidi ktk msimamo wa ligi kuu Bara wakiwa na pointi zao 17 kwa michezo 8 nyuma ya mahasimu wao Yanga SC wanye pointi 19 kwa michezo 7 huku vinara ktk msimamo huo wakiwa ni Azam FC zote za jijini Dar es Saalam.

Jumamosi, 20 Oktoba 2018

Yanga yaiua Alliance Sports Club goli 3 kwa sifuri hii leo uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam.

Mchezo huo uliyokuwa wa vuta nikuvute ikishuhudiwa vijana wa Alliance kujaribu mara kadhaa kuliandama lango la Yanga,lakini hata hivyo juhudi hizo hazikuzaa matunda ambapo mnamo dakika ya 17 ya mchezo H.Makambo aliiipatia Yanga goli la kwanza,huku winga machachali Mrisho Khaphan Ngasa akifunga goli la pili mnamo dakika ya 29 ya mchezo kabla ya mapumziko.Na baadaye kipindi chapili Ibrahim Ajibu Migomba akamaliza kazi kwa kuipatia Yanga goli la 3 dakika ya 86 ya mchezo.

Hadi dakika 90 za mchezo Yanga 3 na Alliance 0

Ijumaa, 19 Oktoba 2018

CHADEMA BADO NI HAI.

HIZI HAPA SERA ZAO KAMA CHAMA:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Chadema bado kimeendelea kijijenga kama chama mbali ya kashikashi zinazopitia kama chama ikiwemo hamahama za baadhi ya waliokuwa Madiwani na wabunge kupitia chama hicho kuamua kijivua nyazifa zao na kukihama chama na kukimbilia chama tawala kwa sababu zao mbalimbali na kubwa hasa ikiwa ni kule kuunga mkono juhudi za serikali iliyopo madarakani inayoongizwa na chama tawala CCM.

Mbali na hayo pia chadema ilipoteza majimbo na kata mbalmbal katika chaguzi za marudio huku chama tawala CCM ikijishindia bafasi hizo huku ikiwatumia viongozi haohao waliyoikimbia Chadema ili kuiwakilisha CCM katika chaguzi hizo.

Chadema kuonesha ni jasiri,wakomavu na wenye nia thabiti kuelekea chaguzi za Serikali za mitaa 2019 na ule uchaguzi mkuu 2020 wameendelea kujijenga na kuanza kuweka wazi sera zao.
Jionee hapa chini.

MANJI RASMI YANGA.

WANACHAMA NA MASHABIKI MENO NJE NJE.
Habari ndiyo hiyo unaambiwa.
Ni kwamba Mara baada ya kujiweka pembeni dhidi ya soka na hasa timu ya Yanga kwa zaidi ya siku 517 ambazo ni sawa na mwaka 1 na miezi 4 na siku 29...,hatimaye Tajiri,mfadhiri,mwenyekiti na kipenzi cha wana Yanga Bw.Yusuph Manji amerejea na kutambuliwa kama ndiye mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe na mabingwa wa kihistoria kunako tasnia ya kandanda nchini Tanzania.

Yusuph Manji alitangaza kujiuzuru kuitumikia Yanga km Mwwnyekiti mnamo mwezi Mey tarehe 20 mwaka 2018.
Kutokuwepo ama kutojihusisha kwake dhidi ya Yanga kuliifanya timu hiyo kuyumba kiasi fulani kiuchumi,kiufundi na hata kushindwa kuutetea ubingwa wao waliyokuwa wakiushikilia kwa matatu mfurulizo hadi mwaka jana.
Mbali hayo timu ilishindwa hata kusafirisha wachezaji baadhi ilipitakiwa kucheza ugenini(mikoani) mfano wa ile mechi kati yao na timu mojawapo ya jijini Mbeya mwaka jana.

Hayo,ni matikeo ya kikao cha kamati ya uchaguzi ndani ya klabu hiyo kilichokaaliwa juzi jumatano  ambapo kilitoka na maazimio ya kumrejesha na kumtambua Manji kama ndiye Mwenyikiti wa timu hiyo huku kamati hiyo ikisisitiza kwamba nafasi zilizowazi na zinazotakiwa kupata viongozi ni Makamu mwenyekiti pamoja nafasi za wajumbe ambao waliyokuwepo awali walijihuzuru nyazifa zao wakiwemo;Salum Mkemi,Hashim Abdallah na Omar Saidi kutoka Tanzania Visiwani(Zanzibar),Huku Ayoub Nyenzi kwa kutohudhuria vikao mfururizo vya kamati hiyo hivyo naye alipoteza sifa za kuwa mjumbe wa kamati hiyo ya Utendaji ndani ya klabu.

Itakumbukwa pia nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa chini ya Clement Sanga aliyejihuzuru nafasi hiyo.

Hata hivyo Katibu mkuu wa klabu hiyo Bw.Omary Kaya alieleza kwamba habari zote kuhusu Mwenyekiti alidai lipo chini ya kamati ya uchaguzi ambayo ndiyo yenye dhamana ya kulisemea hilo huku  mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanga,Bakili Makele alisema kuwa ufafanuzi wa zoezi la uchaguzi na kwamba ni lini utafanyika na habari zote za Manji utatolewa kwenye mkutano na vyombo vya habari muda wowote kuanzia leo Ijumaa.

Wakati hayo yakielezwa na viongozi hao huku wadau,wanachama na mashabiki kindakindaki wa timu hiyo kongwe nchini wameonekana wakifurahia urejeo huo wa bosi huyo kipenzi wa Yanga huku wakitamba kwamba taji la ubingwa ni lao na kwamba wao ndiyo wanastahili kukwea pipa(kupanda ndege)kwenda kuiwakilisha nchi ktk medani za kimataifa.

JIAJIRI MWENYEWE.

UJASIRI NI MALI.
Kwa mahitaji yako yote ya VIATU vya Kimaasai kwa Jumla na rejareja karibu NEW VISION with COMMON SKILLS,DODOMA TZ.

Kwetu utajipatia viatu aina zifuatazo.
(1)Viatu vya kike vya ngozi
(2)Viatu vya kike vya ngozi yenye manyoya.
(3)Viatu vya Kike vya kitambaa
(4)Viatu vya kike vya shanga.
(5)Viatu vya kiume vya ngozi
(6)Viatu vya kike vya shwapa.
Tupigie +255625887699
Whatsapp:+255629108340
Instagram:joachimmkwawa

Jumatano, 17 Oktoba 2018

UJASIRI NI MALI.

JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA KUFULIA YA MAJI.

Leo tena bado tupo hapa kukuhamasisha na kukufunza namna ya kujiajiri wewe mwenyewe.Jifunze tena Fursa hii adhimu.

Sabuni hii ya maji unawezaitumia kwa kudekia sakafu yako,kufulia ama kuoshea vyombo vyako nyumbani.

(1)MAANDALIZI.
(a)Beseni kubwa au Diaba.
(b)kijiko.
(c)Mwiko.

(2)MAHITAJI/MALIGHAFI.
(a)Salphonic acid nusu Lita.
(b)Sless robo Lita
(c)Sodash robo kilo.
(d)Maji Lita 15.
(e)Rangi nusu kijiko.
(f)Sodium salfet nusu kilo
(g)Perfume vijiko 2.
(h)Formaline vijiko 2
(j)Glyceline vijiko 4.

(3)JINSI YA KUTENGENEZA.
(a)Andaa Diaba(jaba)au chombo chochote mfano beseni lenye ujazo wa Lita 20.
(b)Weka maji kwenye chombo hicho na hakikisha chombo chako ni kikubwa kuzidi wingi wa maji yako.
(c)Weka sulphonic acid,sless vyote kama ulivyoelekezwa na kuvipima kwa vipimo tajwa hapo juu.Vichanganye kupata mkorogo ama mchanganyiko mmoja bila kuukoroga lakini ukiwa undani ya jaba lako.
Tia maji yote Lita 15 kwenye jaba na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja yaani kama unakoroga kuelekea kulia usigeuze kuelekea kushoto.
(d)Weka sodash,Rangi uipendayo iwe bluewax,greenwax ama redwax.Tia perfume,Formaline na Glyceline kisha endelea kukoroga mchanganyiko huo kwa dakika 2 au 3.
(e)Chukua chombo kingine cha plastic mfano jagi au bakuli kisha chota huo mchanganyiko wako kiasi halafu utie sodium kwenye bakuli au jagi hilo na ukoroge vizuri.

(f)Kisha mimina mkorogo huo wa kwenye bakuli au jagi kwenye ule mchanganyiko wako wa awali uliyopo kwenye jaba na endelea kukoroga na hapo utaona mchanganyiko unaanza kupanda juu.Hii ina maana kwamba Sodium huingeza wingi wa sabuni yako.

Hivyo ukikoroga Lita 15 hakikisha chombo chako kina ujazo wa Lita 20 au zaidi.
Na Formaline husaidia kuitunza sabuni yako isiharibike haraka yaani ukiweka formaline basi sabuni yako yaweza kaa hata mwaka 1 bila kuharibika.

Baada ya hapo  yaani umemaliza kutengeneza chukua sabuni yako na mimina katika vifungashio ulivyokwisha kuviaandaa,weka lebo yako.Na tayari sabuni yako itakuwa tayari kwa matumizi ama biashara.

Na hii itakuwa ni sabuni safi,nzuri,yenye kunukia,raini isiyochubua mikono ama kufubaza nguo na itakayokuoa matikeo mazuri kwako na sikoni.

Kumbuka.
Zipo aina 5 za Formaline hivyo kuwa makini pindi unapokwenda kununua malighafi zako dukani.Na malighafi hizi hupatikana kwenye maduka maalum ya ujasiriamali tu na vinginevyo.

Aina za Formaline
(1)Formaline ya chakula
(2)Formaline ya kutunzia dawa
(3)Formaline ya kutunzia sabuni
(4)Formaline ya kutunzia maiti
(5)Formaline ya kuzuia wadudu wasiharibu lotion(losheni).

Ahsante sana naomba niishie hapa kwa Leo.
Kesho tena usisite kutufuatilia ili kujuwa tumekuletea kitu gani cha kujifunza kutengeneza na kukufanya ukajiajiri wewe mwenyewe ukajiingizia kipato..

Piga +255625887699

UJASIRI NI MALI:-

JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA KUFULIA YA UNGA.
Ktk ulimwengu wa leo kila kukicha bado mahitaji ya kibinadamu yanazidi kuongezeka.Mahitaji hayo mengi yapo ktk umuhimu mkubwa wa binadamu kutaishi mazingira.

Maisha ya binadamu yanategemeana kati ya binadamu mmoja dhidi ya mwingine.Yaan ili mwanadamu Fulani apate anachohitaji ni lazima ampe binadamu mwenzie naye anachohitaji.

Usafi ni muhimu kila mmoja wetu.Kuoga kwetu ni usafi,kufua nguo zetu ni usafi,kufagia ni usafi pia.Hvy Leo nataka tujikite ktk mafunzo ya utengenezaji wa sabuni ya unga kwa ajili ya mahitaji ya kufulia nguo zetu na mahitaji mengineyo yahusuyo usafi.

Twende pamoja hapa chini.
UTENGENEZAJI WA SABUNI YA UNGA.

(1)MAANDALIZI:
(a)Beseni
(b)Mwiko
(c)Kijiko

(2)MALIGHAFI:
(a)Maji
(b)Sulphonic acid
(c)Sodash
(d)Sodium
(e)Silcate
(f)Nansa
(g)Optical-braytina.
(h)Perfume
(j)Rangi.(Blue wax).

(3)HATUA ZA UTENGENEZAJI:
(a)Pima maji safi Lita 1 tia kwenye Beseni safi.
(b)Pima sulphonic acid Lita 1 na nusu.
Anza kuimimina kwenye beseni lenye maji huku ukikoroga hadi sulphonic acid ijichanganye vizuri katika maji.
(c)Chukua silcate grasi 1 tia kwenye mchanganyiko huo.
(d)Chukua nansa na upime vijiko 5 weka katika mchanganyiko wako na ukoroge tena.
(e)Pima optical braytina vijiko 5 weka katika mchanganyiko wako kisha koroga tena mchanganyiko huo.
(f)Pima sodash kilo 6 weka katika mchanganyiko wako.
(g)Chukua sodium kisha pima kilogram 4,weka katika mchanganyiko wako.
(h)Chukua perfume na upime vijiko 4,weka katika mchanganyiko wako.
(j)Chukua rangi(Blue wax)kisha mimina katika mchanganyiko wako.
Baada ya hapo bila kupoteza muda anza kukoroga ama kuchanganya vizuri mchanganyiko wako kwa kutumia mwiko hadi mchanganyiko huo uwe raini kabisa.

Baada ya hapo anika sehemu safi kivulini.Na ni vizuri ukaianika sebleni ama chumbani palipo pasafi na pakavu..

Baada ya masaa 24,Sabuni yako ya unga itakuwa tayari kwa matumizi ya nyumbani kwako ama kwa biashara.
Weka sabuni yako katka vifungashio,weka lebo yako tayari kwa biashara.Na sabuni yako itakuwa na uwezo wa kudumu mwaka 1 bila kuharibika..

Kujifunza zaidi kwa vitendo,video na picha huna budi kuwasiliana nasi
+255746677970
+255629114323
+255625887699

Ahsante.