Jumamosi, 23 Mei 2020

MTOTO ALIYETUPWA KWENYE SHIMO LA CHOO WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA AOKOLEWA NA JESHI LA ZIMAMOTO.

Ngara Kagera;
Mtoto wa mwaka mmoja aliyetupwa kwenye shimo La Choo cha wasichana shule ya msingi wilayani Ngara mkoani Kagera hatimaye ameokolewa.
Oparesheni hiyo ya uokozi ilifanywa kikamilifu na kufanikishwa kwa Ufanisi mkubwa wa Jeshi La Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania.Jeshi La Zimamoto nchini baada ya kupokea taarifa za tukio hilo La kusikitisha lilifika haraka eneo La tukio na kuanza kazi ya uokoaji mara moja na kufanikiwa kunusuru uhai wa mtoto huyo kwa kumtoa ndani ya shimo kupitia chemba(mfuniko)wa kalo La choo hicho.
Askari wa Jeshi La Zimamoto Constable Denis Minja alizama shimoni humo kwa kamba na kwa ujasiri na ufanisi mkubwa akiongozwa na Jeshi hilo alifanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye kwa kipindi chote alisikika akilia ndani ya shimo hilo.
Kwa ujasiri huo pekee na wa kizalendo hatimaye Kamishina Jenerali wa Jeshi La Zimamoto na Uokoaji nchini Ndugu John Masunga akaamua kumpandisha cheo askari Denis Minja kutoka kuwa Constable hadi cheo cha Koplo.
Sisi kama jamii kwanza tunalipongeza Jeshi letu La Zimamoto na Uokoaji nchini kwa kutimiza vema wajibu wao wa kizalendo katika kushugulikia jambo hilo.Lakini pia tunalaani vitendo viovu na vya kinyama kama hivi vya watu(wazazi/walezi)kuchukua sheria mkononi na kutekeleza matukio yasiyo ya kibinadamu kama haya.Sambamba na kuwaasa Watanzania kuwa na hofu ya Mungu na kwamba ni kosa kisheria kutishia ama kukatisha uhai wa wengine kinyume na sheria zetu nzuri na bora zinazompa Mtanzania Uhuru na haki ya kuishi kwani kwa kufanyaje hivyo ni kupoteza nguvu kazi ya kesho kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.

Jumamosi, 16 Mei 2020

HIZI HAPA FURSA 5 ZA KIBIASHARA ZINAZOHITAJI MTAJI MDOGO

Habar za wakati huu ndugu msomaji,mjasiriamali na maana jukwaa mwenzangu wa jukwaa pendwa la UJASIRI NI MALI(JIAJIIRI).
Hongera sana kwa mfungo wa Ramadhan,hongera kwa mapambano dhidi ya Covid-19.Na lakini pia hongera kwa kuendelea kuchakalika kimaisha ukiwa nyumbani.
Najuwa kila mtu anapambana katika shughuli mbalimbali ili kujipatia kipato.Yamkini unajiuliza leo mimi na jopo langu tumekuletea nini mezani??.
Basi leo kama kawaida yetu tunapenda kukuona wewe mjasiriamali ukiwa juu kibiashara na kipato.
Leo tumekusogezea fursa 5 muhimu za kibiashara ambazo zinahitaji mitaji midogo sana ili kuzianzisha/kuzifanya.
Angalia video hii mwanzo hadi mwisho naamini utajifunza zaidi.
Usisite kuja YouTube channel yetu iitwayo Mnyausi TV ili upate video mbalimbali za mjasiriamali.SUBSCRIBE Channel yetu(Mnyausi TV),Like,Comment na ku Share.
By
Joachim Mkwawa.