Jumanne, 3 Julai 2018

JIFUNZE KUTENGENEZA VIATU VYA KIMAASAI.

UJASIRI NI MALI(JIAJIRI).
Viatu vya Culture maarufu km viatu vya Kimaasai ni hitaji kubwa sana kwa watu hasa ukanda wetu huu Afrika Mashariki.Ni viatu pendwa mno na huvaliwa watu rika na jinsia zote.
Mahitaji ya viatu hivi yanaonekana kuwa makubwa hasa kutokana na ukwel kwmb,kwanza hamchoshi mvaaji,havina wakati wala mahala pa kuvivalia,huvaliwa na mtu yeyote kwa rangi yoyote ya nguo.Huvaliwa na kumpendeza kila anayeamua kuviavaa iwe kwa kushindia ama kwa kutokea.
Pili huuzwa gharama nafuu na hudumu muda mrefu iwapo utavinunua vikiwa bora,imara na kutunzwa vizuri.

Historia inaonesha kwmb viatu hivi vilianzakutengenezwa nchini Rwanda na hatimaye kuenea zaidi kanda ya Kaskazini mwa Tanzania vikiletwa na watu wa Kenya.
Viatu hv vilipewa jina la "Viatu vya Kimaasai",kwa sababu vinauzwa sana na jamii ya Wamaasai hasa nchini Tanzania...,na watu wengi hudhani ama kuamini kwmb Wamaasai ndiyo watengenezaji wa viatu hivi lkn ukwel ni kwamba Viatu hv havitengenezwi na Wamaasai na km wapo basi ni wachache sana.Badala yake viatu hv hutengezwa na watu wengine kabisa na Wamaasai wao ndiyo huvilangua kwa bei za jumla na kuanza kuvitembeza sehemu mbalimbali wakiviuza.Hvy kutokana na mara nyingi na sehemu nyingi unakutana na Wamaasai ndiyo wanaoviuza viatu hivi basi ndiyo maana likaja jina la viatu vya Kimaasai na ikakaririwa hivyo.

NINI FAIDA YA VIATU HIVI KWA MTENGENEZAJI.
Yah zipo faida nyingi sana kwa yeyote atakayeamua kuwekeza ktk mradi ama fursa hii ya viatu.
(1)Hukupa uhakika wa kipato muda wote utakapokuwa ukijihusisha navyo(kuvitengeneza).
(2)Hukutambulisha vema mbele ya wajasiriamali wengine,wachuuzi,wafanyabiashara wa viatu na mavazi,wateja wa rejareja na mataasisi mengineyo hasa ya mikopo mambo mengine kibao ya ujasiriamal na uwekezaji.
(3)Mwanzo wa kumiliki biashara yako na kiwanda chako binafsi.
(4)Unawezakuwa mwajiri mpya wa wengine hasa vijana na ukaisaidia serikali ktk kupunguza wimbi la watu wasiyo na ajira coz wapo watakaoajiriwa nawe kiwandani direct na lkn pia wapo watakaojiajiri wenyewe kwa kulangua mzigo kwako na wao wakaenda kuuza kwa watumiaji.
(5)Utaweza kuyamudu maisha yako ya kila cku kutokana na kupata kipato binafsi na chenye uhuru wa kukiamulia matumizi.
(6)Utatimiza malengo yako,ndoto na maono yako vile utakavyo mwnyw.
(7)Utajivunia kuwa mzalendo kwa kutumia malighaf za ndani ya nchi yako,ukazalisha na hvy utalipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa lako.

SOKO LIKOJE?.
Ndiyo,
Soko la bidhaa hii lipo na ni kubwa tena lisilo na ukomo wa muda coz kila cku watu huvaa na hutaka wapendeze.Ikumbukwe kuwa viatu si sawa na nguo.

Mtu anaweza chanikiwa na nguo lkn akaishona ama akadumu nayo hata miaka miwili hadi mitatu lkn viatu huwa ni hitaji la kila cku.
Mtu hawezi katikiwa na kiatu mbele za watu na akamudu kutembea peku ilihali muuza viatu upo jirani tofauti na nguo.
Hvy soko lipo.Viatu hv unawezauza kwa jumla ama rejareja kwa mifumo utakayoiona ww kuwa inafaa.
Wapo wateja wanaonunua na kwenda kuvikopesha kwa watu wao huko majumbani,wengine hununua na kwenda kuviuza kupitia maduka yao ya nguo na viatu,wengine hununua na kwenda kuvichuuza minadani,magulio ama kutembeza mitaani na lkn pia wapo ambao huvinunua na kuvivaa wao binafsi.
Viatu hv pia vimeanza kuingizwa mataifa mengine ya nje ya Afrika Mashariki kutokana na wageni wengi wanaoingia na kutoka ktk ukanda huu pale wanapokutana navyo wakavinunua na kuvivaa wameonekana wakipendeza sana na pia hata wanapowachukulia na kuwapelekea wapendwa wao huko ktk mataifa yao bado vimeonekana kuwapendeza na kuwatia hamasa ya kuona kuna umuhimu wa kuvichukuwa huku Afrika na kuvipeleka kwao.

Mfano binafsi mnamo mwezi wa nne 2018 niliuza vuatu pea 32 vikaenda nchini Finland na aliyevipeleka aliwasiliana nami kwa Email kwmb aliviuza kwa muda mfupi sana na kwa pesa nzuri baada ya kuvifikisha kule.Akiahidi akiwa anarejea nchini Tanzania atanijuza nimtengenezee mzigo mwingine mkubwa na mzuri zaidi.
Hvy hii inaonesha ni jinsi gani kitu kidogo kwetu kinavyochukuliwa uzito mkubwa kwa wenzetu.

Hii ni fursa,idake,ikamate sawasawa,itafakari,ichanganue,ifanyie tafiti za kutosha na uchuwe hatua zaidi kuifanyia kazi..

KUNA AINA NGAPI ZA VIATU HIVI?
Yap,
Zipo aina kama 7 hivi za viatu hivi vya Culture(Kimaasai)
(1)Viatu vya ngozi pure
(2)Viatu vya ngozi yenye manyoya
(3)Viatu vya kitambaa
(4)Viatu vya Shanga kawaida
(5)Viatu vya shanga makirikiri
(6)Viatu vya shwapa/leather
(7)Viatu vya kufumwa kwa nyuzi.

Aina hizo 7 hutokana utofauti wa kimwonekano,ubora na matumizi ya malighafi tofauti tofauti zitumikazo kuvitengeneza viatu kulingana na eidha mahitaji ya soko ama mapendekezo(mapenzi)ya fundi tu mwenyewe.

UPATIKANAJI WA MALIGHAFI NA VIFAA UPOJE?
Twende kazi.
Aise upatikanaji wa malighafi hapa nchini Tanzania siyo mkubwa sana hasa kwa mikoa iliyo mbali na Arusha  ama kanda ya kati.
Lkn kwa mikoa km Arusha,Mwanza,Dodoma,Mbeya,Morogoro,Tanga na Dar es Saalam malighafi hizi zipo isipokuwa siyo kwa uwazi na wepesi sana km ilivyo sukari,chumvi ama unga kwny maduka mbalimbali kutokana na watumiaji wa malighafi zenyewe kuwa siyo wengi,yaani wanaojihusisha na utengenezaji wa viatu hivi siyo wengi mno.Hvy ili kuzipata inakulazimu kuulizia hasa kwa mafundi wa kushona viatu(Shoe shiners) wao watakuonesha ni wapi hununulia mahitaji yao hasa soli za kurepair viatu,kiwi,uzi nk kwani wanakonunulia vitu hivyo ndiko na malighafi hizi hupatikana ingawa siyo kwa mikoa yote km nilvyoeleza hapo juu.

Kuhusu vifaa pia vipo ktk maduka ya vifaa ya magari,mashine,ushonaji,ujenzi na maduka ya wajasiriamali wa bidhaa hii ya viatu.
Vifaa hivi ni pamoja na
>>Nyundo
>>Mikasi
>>Plaizi
>>Kinoo(Jiwe la kunolea)
>>Kisu(Patasi)
>>Purnch numbers
>>Purnch za kutobolea matundu
>>Magongo(Miguu bandia)
>>Size za miguu
>>Rula
>>Kalamu maalum(Silver pen)
>>Sindano
Nk.

Malighafi ni km vile
>>Gundi
>>Soli
>>Bango(box)
>>Shwapa/leather
>>Kitambaa(Valvet)
>>Kisigino(top up)
>>Pipe(Bomba)
>>Kamba(gidam)
>>Ribit
>>Michoro ya maua
>>Dawa(Leather clear na Dai)
>>Rubber band(vifungashio).

Naomba niishie hapa kwa leo.
Usisite kunifuatilia hapa hapa ktk chimbo lako la nguvu mnyausiblog.blogspot.com.
Au tembelea instagram jina Joachim Mkwawa.
Email:joachimmkwawa8@gmail.com
Au whatsapp namba +255629108340
Piga 0629114323/0746677970.

Ili ujifunze zaidi namna kutengeneza pesa kuputia fursa hii kwa kulipia ada kidogo tu itakayokupa kipato cha uhakika maishani mwako.

NB
UJASIRI NI MALI(JIAJIRI).
©Joachim L Mkwawa
New Vision with Common Skills.
Dodoma Tanzania