Ijumaa, 20 Januari 2017

UPENDO NI TIBA KWA NAFSI ILIYOJERUHIWA.

Habari za siku,kheri ya mwaka mpya 2017. Natumai muwazima nyote wasomaji wetu. Awali ya yote tuwatake radhi kwa kutokuwepo hewani kwa muda kutokana na maboresho tulokuwa tukiyafanya ktk blog yetu ili kuifanya iwe na muonekano mzuri,wa kuvutia na wenye kubeba uhondo bora na wa kuaminika ili kukidhi mahitaji yenu wasomaji wetu. KARIBU TUJIFUNZE. Upendo~Ni ile hali ya kuthaminiwa,kutunzwa,kulindwa,kutetewa na kutimiziwa mahitaji muhimu.Upendo hupimwa kwa mambo mengi kulingana na mahitaji ya muhitaji lkn baadhi yake ni hayo niloyataja hapo juu.Upendo ni moja kati ya viungo vya tunda la Roho.Upendo hujenga,hukuza,na kumuendeleza mtu. Palipo na upendo pana Amani,heshimaTumaini,huruma,na mafanikio.Upendo huwaleta watu karibu,hujenga mshikamano na ushindi utokanao na umoja ndani yake. Pasipo upendo pana machafuko,chuki,mateso na unyanyasaji maishani.Lkn penye upendo pana jawabu hata ktk kile kilichoshindikana.Ili pawepo upendo,..lazima hekima iwepo,utu wema,uvumilivu,utulivu wa nafsi,nk. Upendo humpa tumaini aliyekata tamaa. Upendo humpa furaha aliye na simanzi. Upendo humpa tiba aliyejeruhiwa nafsi. Upendo huleta mafanikio maishani. Upendo huleta amani idumuyo. Upendo humjengea mtu uzalendo. *2Korintho 7:1 hadi mwisho Tumeagizwa upendo,hvyo tupendane.Ucmbague mtu kwa rangi,kabila ama udhaifu wake maana hujui amebeba sehemu gani ya maisha yako. Ukipenda,nawe utapendwa.Ukitenga au kubaguwa nawr utatengwa na kubaguliwa.Ukipenda utaheshiwa,utafurahiwa na wakati mwingine utasaidiwa na kutetewa hata wakati umetenda makosa. Leo tuishie hapo.